Shaffih Dauda 'Al Ahly ni Levo Nyingine, Haya Tunayoshangaa ndio Mafanikio Waliyotuzidi'

Shaffih Dauda 'Al Ahly ni Levo Nyingine, Haya Tunayoshangaa ndio Mafanikio Waliyotuzidi'

 

Haya tunayoyashangaa ndio mapungufu yetu, timu ina vitengo zaidi ya 20 na kila mmoja kwenye idara yake anatakiwa ajiandae, kuna mtu kazi yake ni kuhakikisha timu inasafiri, wakifika wapate huduma kwa wakati ili timu isichelewe.


Yupo mwingine wa recovery ameshafanya utafiti mfano Tanzania ni vitu gani vinapatikana, hiki hakipo maana yake lazima nije nacho, ndio hii unaona watu wanakuja na kila kitu, sisi tunawashangaa wamekuja na mapipa.


Wamekuja Vipers hawakubeba mapipa, wamekuja Rivers United hawakubeba kuna watu ambao wameshajitofautisha na wametengeneza level.


Al Ahly ni level ya klabu zinazocheza Ulaya, kwa Ulaya kutoka England kwenda Italy miundombinu yote ipo sawa, Ahly wapo Afrika lakini wanaishi kimbele na ndio maana kuna muda unalinganisha mchezaji wa Ahly analipwa kiasi gani? Kwamba kuna wachezaji wanalipwa mshahara hadi milioni 200 kwa mwezi.


Katika mazingira ya kawaida sisi tumefika level ya kumlipa mchezaji milioni 300 kwa mwezi?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad