Simba Wapata Suluhisho Baada ya Hofu ya Kumkosa Beki Kisiki Inonga, Ramani iko Hivi

 

Simba Wapata Suluhisho Baada ya Hofu ya Kumkosa Beki Kisiki Inonga, Ramani iko Hivi

Simba iko mawindoni ikijiandaa na mchezo wa African Footbal League dhidi ya Al Ahly ya Misri, lakini hofu kubwa ni uwezekano wa kumkosa beki Henock Inonga ambaye ni majeruhi, lakini Wanamsimbazi wameambiwa watulie kwani hakuna cha kuhofia kwa vile wana kitasa kingine, Kennedy Juma.

Mchezo huo wa ufunguzi wa michuano ya African Football League (AFL) utachezwa Oktoba 20 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kisha kurudiana Oktoba 24 jijini Cairo, Misri.

Beki wa zamani wa Kagera Sugar, George Kavila aliliambia Mwanaspoti, Simba haina sababu ya kuwa na hofu kwani uwepo wa Kennedy na mabeki wengine kunatosha, sababu kitasa huyo amekuwa na kiwango bora tangu alipoumia Inonga akikiwasha kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.

Kavila ambaye kwa sasa anasomea ukocha akiwa na Leseni C ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), alisema kinachombeba Kennedy ni nidhamu na utayari wake muda wote anapohitajika kuipambania timu, hivyo ana imani kubwa kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly atafanya vizuri.

“Kennedy (Juma) ni mchezaji mzuri ndiyo maana yupo Simba na ni mwaka wa tatu kama sikosei hii ina maana kuwa ni mchezaji mzuri na anaaminiwa. Naamini atacheza vizuri kama ambavyo amekuwa akicheza kila anapopata nafasi,” alisema Kavila.

“Amecheza vizuri, ameziba nafasi vizuri na mechi zote ambazo amecheza timu imecheza vizuri kwa maana wamepata matokeo. Kinachombeba nafikiri anajitambua, ana nidhamu na anajiweka tayari muda wote anapokuwa anakosa nafasi ya kuanza katika timu.”

Akizungumzia vitu ambavyo Simba inapaswa kuvifanyia kazi kuelekea mchezo huo alisema: “Wana benchi zuri la ufundi nafikiri wameyaona makosa na watayafanyia kazi, Al Ahly ni timu kubwa Afrika unapocheza nao usifanye ama upunguze makossa, umakini tu unahitajika na siyo kwa mabeki tu bali kwa timu nzima.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad