TFF yaificha Taifa Stars

 

TFF yaificha Taifa Stars

Timu ya taifa ya Tanzania taifa stars itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Sudan, kipindi hiki cha kalenda ya kimataifa ya FIFA. Mchezo huu utachezwa nchini Saudi Arabia, TFF imethibitisha.

Baada ya maswali mengi kuhusu ratiba ya Taifa stars itacheza dhidi ya timu gani na wapi. Hatimaye Shirikisho la soka nchini TFF limethibitisha kuwa Taifa Stars itacheza dhidi ya timu ya taifa ya Sudan mchezo wa kirafiki na mchezo huo utachezwa nchini Saudi Arabia. 

TFF wamethinitisha taarifa hiyo kupitia mitando ya kijamii baada ya kuposti picha za wacheza wakiwa kwenye mazoezi. Taarifa iliyotolewa na TFF kupitia mitando ya kijamii ilisema 

“Kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars” kimeanza mazoezi kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Sudan, utakaochezwa Saudi Arabia.”

Licha ya wachezaji kuonekana wakiwa wanafanya mazoezi lakini bado kikosi cha nyota wanaounda kikosi cha Taifa Stars hawajatangazawa ni wangapi na ni kinani. Inaripotiwa kuwa kikosi hicho kitaondoka nchini leo kwenda Saudi Arabia.


 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad