Tyson Fury Hakustahili Ushindi Mbele ya Francis Ngannou

 

Tyson Fury Hakustahili Ushindi Mbele ya Francis Ngannou

Usiku wa kuamkia leo Bingwa wa dunia wa uzito wa juu wa [WBC ]Tyson Fury alimshinda bondia wa zamani wa [UFC ] Francis Ngannou kwa uamuzi wa Majaji wawili kwa mmoja katika pambano lisilo la ubingwa lililochezwa nchini Saudi Arabia .Pambano ambalo watu wengi waliamini Ngannou alistahili ushindi.


Ngannou alimwangusha Tyson katika raundi ya tatu kwa [ left hook ] ingawa haikuamua mwenendo wa pambano kwa asalimia kubwa lakini ni kama pambano lote lilitawaliwa na Ngannou kwa ambao tumeangalia pambano hilo hata ukiuliza zaidi ya mara tatu bado Ngannou alistahili kushinda .


Jaji wa kwanza alitoa [95-94 ] kwa Ngannou , Majaji wengine walitoa [96-93] na [95-94 ] kwa Fury


Maoni ya wadau wakubwa wa mchezo wa ngumi wanaamini kwamba mechi hiyo ilipangwa kwa ajili ya Fury kushinda.


Bondia Tyson Fury ana pambano la ubingwa wa uzito wa juu dhidi ya Oleksandr Usyk mjini Riyadh katika tarehe ambayo bado haijatangazwa rasmi lakini huwenda ikawa Desemba 23.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad