Uamuzi kesi ya akina Mdee Disemba 14





MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga tarehe 14 Disemba 2023 kutoa uamuzi wa kesi iliyofunguliwa na wabunge viti Maalum 19 wakiongozwa na Halima Mdee, kupinga kufukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Tarehe hiyo imepangwa leo tarehe 23 Oktoba 2023 na mahakama hiyo jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Cyprian Mkeha, baada ya pande zote mbili kufanya mawasilisho ya mwisho.

Akizungumza baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Wakili wa Mdee na wenzake, Edison Kilatu, amedai siku hiyo mahakama itaamua kama wateja wake wamefukuzwa kihalali au la.

“Kwa ujumla leo tunakuja kwa ajili ya kupata maelekezo ya mahakama juu ya tarehe ya kufanya maamuzi, Jaji baada ya vitu alivyoagiza vifanyike kufanyika ambavyo ni mawasilisho ya mwisho, mchakato umekamilika na ameagiza tarehe 14 Disemba 2023 saa nane na nusu mchana itakuwa tarehe ya hukumu,” amedai Kilatu na kuongeza:


“Siku hiyo mahakama itaamua kama walifukuzwa kihalali au kinyume Cha sheria, kama itabaini walifukuzwa kinyume Cha sheria maana yake maamuzi ya Chadema ni batili na wataendelea kuwa wanachama.”

Katika kesi hiyo ya  madai Na. 36/2022, Mdee na wenzake wanaiomba mahakama ifanye mapitio ya kisheria kuhusu mchakato uliotumiwa na Chadema kuwavua uanachama, wakidai ulikuwa kinyume cha sheria.

Katika utetezi wao, wabunge hao wakidai mchakato huo ulikuwa batili kwa kuwa hawakupewa nafasi ya kusikilizwa, ulikuwa na upendeleo pamoja na maamuzi kufanyika kwa shinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi.


Hata hivyo, Chadema kilikanusha madai hayo kikisema kiliwapa nafasi ya kujitetea lakini waligoma kuitumia, kwa kuwa walipewa wito wa kufika mbele ya kikao Cha Kamati Kuu kilichopangwa kwa ajili ya kuwahoji, lakini hawakuitikia.

Mbali na Mdee, miongoni mwa wabunge wengine waliofungua kesi hiyo ni, Cecilia Pareso, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Nusrat Hanje, Ester Bulaya na Esther Matiko.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad