Unaambiwa Upo Uwezekano Mkubwa Kwa Simba na Yanga Kukutana (Kariakoo Derby) Ligi ya Mabingwa
Hii ni kutokana na Simba SC na Yanga SC kupangwa kwenye vyungu tofauti kuelekea droo ya makundi ambayo inatarajiwa kuchezwa Oktoba 6, 2023 mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Simba SC imepangwa kwenye chungu namba 2 sambamba na CR Belouizdad ya Algeria, Pyramids ya Misri na Petro Atletico ya Angola. Kwa upande wake Young Africans SC wamepangwa kwenye chungu namba 3 sambamba na TP Mazembe ya DRC, Al Hilal SC ya Sudan na Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Tofauti na kanuni za upangaji wa makundi barani Ulaya, kwa upande wa Afrika hakuna kizuizi cha timu mbili kutoka Taifa moja kupangwa kwenye kundi moja CAFCL.
Kanuni ya 3 ibara ya 17 ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kila kundi litaundwa na timu moja kutoka kila chungu kati ya vinne, hakuna zuio kwa timu mbili za nchi mmoja kukutana. “Chama cha mpira hakiwezi kuwa na timu zaidi ya mbili kutoka nchini mwake kwenye hatua ya makundi” inafafanua kanuni hiyo.
VYUNGU (POTS) KUELEKEA DROO YA MAKUNDI CAFCL
POT 1.
🇪🇬 Al Ahly
🇲🇦 Wydad
🇹🇳 Esperance
🇿🇦 Mamelodi
POT 2.
🇩🇿 Belouizdad
🇪🇬 Pyramids
🇦🇴 Petro Atletico
🇹🇿 Simba SC
POT 3.
🇹🇿Yanga SC 🇹🇿
🇨🇩 TP Mazembe
🇸🇩 Al Hilal SC
🇨🇮 ASEC
POT 4.
🇹🇳 Etoile Sahel
🇧🇼 Jwaneng Galaxy
🇲🇷 FC Nouadhibou
🇬🇠Medeam
✍️ Nini maoni yako kuhusu uwezekano wa uwepo wa derby ya Kariakoo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika?