Waalgeria Wamtimua Kocha SVEN Kabla ya Kukutana na Yanga



MWEZI mmoja tu kabla ya CR Belouizdad ya Algeria kuivaana na Yanga kwenye mechi ya kwanza ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mabosi wa timu hiyo wamemtimua kocha mkuu, Sven Vandenbroeck, ikiwa ni miezi mitatu tu tangu alipotua klabuni hapo akitokea Wydad Casablanca ya Morocco.

CR Belouizdad imepangwa na kundi moja la D pamoja na timu za Medeama ya Ghana na Al Ahly Misri na itaanza mechi ya kwanza ikiwa nyumbani Novemba 25 kukaribisha Yanga, lakini mapema jana mchana uongozi wa klabu hiyo umetoa taarifa kuwa wamekubaliana na kocha huyo kusitisha mkataba baina yao.

Kocha huyo wa zamani wa Simba alijiunga na miamba hiyo, Julai mwaka huu baada ya kuachana na klabu ya Wydad ya Morocco na hatua hiyo imekuja saa chache tu tangu mabingwa hao wa Algeria kufungwa mabao 3-2 na Khenchela katika mechi ya Ligi Kuu.

Sven aliyeinoa Simba kuanzia Desemba 2019 hadi Januari 2021, aliondoka baada tu ya kuipeleka timu hiyo makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia ushindi wa jumla wa mabao 4-1, dhidi ya Platinum of Zimbabwe.

Kuondoka kwa kocha huyo mzoefu na soka la Afrika katika ardhi ya Tanzania haikuchukua muda mrefu kupata tena timu ya kuifundisha kwani ilimchukua siku mbili kukaa bila kazi kisha kuajiriwa AS FAR ya Morocco na Julai 2022 alijiunga na miamba ya Saudi Arabia klabu ya Abha kabla ya kutimuliwa Oktoba 8, mwaka huo baada ya kufungwa 3-0 na Al-Nassr.

Mei mwaka huu aliajiriwa Wydad kabla ya kuondoka Julai baada ya kuingoza mechi 11 na kutua CR Belouizdad na kuiongoza mechi nne tu, zikiwamo mbili za Ligi ya Mabingwa na nyingine za Ligi Kuu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad