Wakili ‘Feki’ Akamatwa Baada ya Kushinda Kesi 26

Wakili ‘Feki’ Akamatwa Baada ya Kushinda Kesi 26


Mamlaka nchini Kenya zinamshikiria Brian Mwenda, anayedaiwa kuwa wakili ‘feki’ ambaye kwa zaidi ya miaka kumi amekuwa akijitambulisha kama Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya na Mwananchama wa Chama cha Wanasheria cha Kenya (LSK), tawi la Nairobi.


Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari nchini humo zinasema ‘wakili’ huyo ameshinda kesi 26 mbele ya Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu na Majaji wa Mahakama ya Rufani kabla ya kukamatwa.


Mwenda amekamatwa na LSK Nairobi, ambapo imeelezwa kuwa katika taarifa za Mawakili zilizopo LSK, zinaonyesha kuwa licha ya kuwa jina la Mwenda halipo katika orodha hiyo, pia hana leseni.


Sheria za Kenya zinamtaka kila wakili kuwa leseni hai ambayo kwayo anaruhusiwa kufanya kazi ya Wakili. Kwa mantinki hiyo, kwa kuwa hakuna na leseni, hivyo hawezi kuwa Wakili wa Mahakama Kuu nchini humo, lakini pia hawezi kuwa mwanachama wa LSK.


Tawi LSK Nairobi limesisitiza dhamira yake ya kulinda uadilifu na weledi wa taaluma ya sheria na kuwaepusha wananchi dhidi ya vitendo vya udanganyifu.


Hata hivyo baadhi ya watu kwenye mitando ya kijamii, wamekuwa wakimpongeza kwa ujasiri na kujiamini huku aliyewahi kuwa Gavana wa Kaunti ya Nairobi, Mike Sonko, akijitolea kumfadhili katika masomo ya sheria.


Kwa mujibu wa mtandao wa The Daily Post, Mwenda anadaiwa kujifanya wakili ili hali hajaudhuria mafunzo yeyote ya sheria huku akishinda kesi 26.


Katika ukurasa wake kwenye mtandao wa X, Sonko amesema atamfadhili Mwenda ili asomee shahada ya sheria.


“...ikiwa atakosa pesa, basi mimi nitamfadhili kwenda Shuke ya Sheria Kenya, mtu huyu amekuwa mtetezi, hakuwahi kwenda shule yoyote ya sheria...ana mafanikio kwa kushinda kesi 26 mbele ya Mahakimu, Majaji wa Mahakama Kuu na Majaji wa Mahakama ya Rufani hadi alipokamatwa leo,” Sonko amesema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad