Wakili Mwabukusi Aitwa Polisi Tena, Adaiwa Kufanya Mkusanyiko Usio Halali



Jeshi la Polisi limemtaka Wakili Boniface Mwabukusi kuripoti katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa huku likitaja sababu ni kuhutubia Mkusanyiko usio halali

Oktoba 8, 2023 Wakili Mwabukusi na Dkt. Wilbroad Slaa walipanga kuhutubia Mkutano ambao ulizuiwa na Polisi na baadaye alielekea Kijiji cha Kandete ambako amedaiwa kuhutubia bila kuwa na Kibali

Leo Oktoba 9, 2023 Wakili huyo alitangaza kufanya Mkutano na Waandishi wa Habari hata hivyo Wakili anayemtetea Mwabukusi, Philip Mwakilima amesema Mkutano hautafanyika baada ya Wahusika kuitwa Ofisi ya Upelelezi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad