Wakili Mwabukusi Yamkuta ya Fatma Karume, Uwakili wake Hati hati

 

Wakili Mwabukusi Yamkuta ya Fatma Karume, Uwakili wake Hati hati

Wakili Mwabukusi Yamkuta ya Fatma Karume, Uwakili wake Hati hati

Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Eliezer Feleshi amewasilisha malalamiko Kamati ya Maadili ya Mawakili, dhidi ya Wakili Boniface Mwabukusi.


Kupitia samasi iliyotolewa juzi na kusainiwa na kamati hiyo, Faraji Ngukah shauri hilo litasikilizwa Novemba 20 na 21, mwaka huu.


“Kamati itakaa Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi Kivukoni, Dar es Salaam, saa 3.00 lazima ujiandae kwa ajili ya kusikiliza shauri, kama hutofika shauri litaendelea,” ilieleza sehemu ya samasi hiyo.


Alipotafutwa na Mwananchi kuzungumzia samasi hiyo, Mwabukusi alisema kosa analodaiwa kutenda ni ukiukaji wa maadili na kwamba hakuna kinachoweza kumtisha.


“Wanasema nimekiuka maadili ya uwakili, kwa hiyo mwanasheria mkuu anataka nifutwe nisiwe wakili, hakuna kinachonitisha.


“Nilijua lazima unapokuwa kwenye Serikali au taasisi zetu unapoziambia ukweli halafu zimezoea kuwaona wananchi kama wajinga, lazima uwe tayari kwa litakalotokea,” alisema.


Mwabukusi alisema haogopi cheti chake cha uwakili kuchukuliwa, akisisitiza hata cheti chake cha darasa la saba kimetolewa na Serikali, hivyo nacho kinaweza kuchukuliwa.


Alisema yupo tayari kuthibitisha chochote alichozungumza na atahitaji shauri hilo kuendeshwa kwa uwazi.


Mwabukusi si wa kwanza


Yanayotokea kwa Mwabukusi yaliwahi kumfika Fatma Karume, ambaye mgogoro wa uwakili wake ulianzia katika mwenendo wa kesi ya kikatiba namba 29 ya mwaka 2018.


Kesi hiyo ilifunguliwa na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu akipinga kuteuliwa kwa Profesa Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akidai hakuwa na sifa, lakini Serikali ilimwekea pingamizi la awali.


Akijibu hoja za pingamizi hilo, pamoja na mambo mengine, Fatma alidai Profesa Kilangi bado ni mchanga kitaaluma, hana uwezo wa kusimamia jukumu la uwanasheria mkuu wa Serikali na amekuwa akiipotosha Serikali katika mambo mengi.


Kutokana na kauli hizo, Wakili Mkuu wa Serikali aliwasilisha malalamiko kwamba kauli hizo ni kinyume na kanuni za maadili ya mawakili, ni kejeli na kashfa ya kudhalilisha ofisi ya AG.


Kutokana na malalamiko hayo, Septemba 20, 2019 Jaji Kiongozi, Dk Eliezer Feleshi alimsimamisha Fatma Karume kwa muda kutoa huduma za uwakili na baadaye aliondolewa kwenye orodha ya mawakili.


Hata hivyo, Fatma alipokata rufaa Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na jopo la majaji watatu, Issa Maige (kiongozi wa kopo), Dk Deo Nangela na Edwin Kakolaki Juni 21, 2021, ilibatilisha uamuzi wa Kamati ya Mawakili kutokana na hoja ya pingamizi iliyowasilishwa.

Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad