Watu 20 Wafariki Ajalini Tabora

Watu 20 Wafariki Ajalini Tabora

Watu wapatao ishirini wamefariki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori mjini Nzega.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai ameeleza akiwa mjini Sikonge leo Jumamosi Oktoba 21, 2023; kuwa katika ajali hiyo iliyotokea muda mfupi uliopita watu ishirini wamefariki dunia.

Amesema kwa sasa anaelekea eneo la tukio kufahamu zaidi kuhusu ajali hiyo na namna majeruhi wa ajali watakavyopata huduma na miili kuhifadhiwa.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Nzega alikuwa katika maadhimisho ya miaka 100 ya Hospitali ya Misheni inayomilikiwa na Kanisa la Moravian, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao amesema ajali hiyo imehusisha basi la Alpha linalofanya safari zake kati Shinyanga na Dar es Salaam, na kwamba wakati wa ajali, lilikuwa likitokea Shinyanga.

"Nimepata taarifa hiyo na sasa ndio naelekea eneo la tukio na taarifa kamili nitaitoa baada ya kufika na kujua hali ilivyo," amesema

Hii ni ajali kubwa kuua idadi kubwa ya watu katika Mkoa wa Tabora kwa mwaka huu.

Taarifa zaidi endelea kufuatilia tovuti ya Mwananchi na mitandao yake ya kijamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad