Yanga; 'Thank You' Konkoni, Welcome 'Goal Machine'

 

Yanga; 'Thank You' Konkoni, Welcome 'Goal Machine'

Mabosi wa Yanga wanakutana kufikiria watapitaje kwenye mechi sita za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Lakini mastaa wawili wenye heshima Jangwani wamesema kwa vile Hafiz Konkoni aliyesajiliwa kama mbadala wa Fiston Mayele ameshindwa kupiga kazi, angefyekwa mapema kwenye dirisha dogo ili aletwe mshambuliaji wa maana.


Kama hujui kwenye mabao 15 ambao Yanga ni mawili pekee yaliyofungwa na washambuliaji halisi ambao ni Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni.


Mabao mengine 11 yamefungwa na viungo, Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Sterphanie Aziz KI  kila mmoja  matatu, Mudathir Yahaya akifunga mawili huku mabeki Dickson Job na Yao Kouassi kila mmoja akifunga bao moja.


Takwimu hizo zikawaibua kiungo mshambuliaji wa zamani, Sekilojo Chambua aliyeliliambia Mwanaspoti katika dirisha dogo la usajili linalokuja lazima mabosi wao warudi sokoni kusaka mshambuliaji.


Chambua alisema licha ya uongozi wa klabu yao kumsajili Konkoni bado ameshindwa kukidhi kiwango ambacho klabu yao ilitarajia na  anaweza kupisha ingizo jipya ambalo uongozi wao utafanikiwa kumpata mtu mpya.


“Unajua ukweli ni kwamba bado hatujapata mtu kama Mayele (Fiston) nafahamu hatuwezi kupata mtu wa kariba yake, lakini timu ilikuwa inahitaji angalau kuona mtu ambaye atakuja na ubora wake na kuendelea kufunga,” alisema Chambua na kuongeza;


“Nadhani viongozi wanatakiwa kurudi sokoni kutafuta mshambuliaji mpya, timu inahitaji mtu anayejua kufunga hiyo ndio kazi ya mshambuliaji, tunahitaji kuwa na mtu ambaye akipata nafasi tatu basi anaweza kufunga mbili au angalau moja.”


Chambua aliongeza wakati Yanga ikipiga hesabu za kucheza mechi za makundi mshambuliaji huyo atakuja kuongeza nguvu kuanzia hapa ambapo viungo wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kufunga.


“Sio kwamba tangu aondoke Mayele timu haifungi, timu ina rekodi nzuri ya kufunga lakini mshambuliaji mzuri atakuja kuongeza ubora zaidi wa makali ya kikosi wakati huu viungo wakiendelea kufanya mambo makubwa,” alifafanua Chambua.


Wakati Chambua akiyasema hayo ligendi mwingine ambaye ni winga, Edibily Lunyamila alisema usajili wa mshambuliaji mpya mwenye ubora utakuja kuwapunguzia presha Mzize na Musonda.


“Timu inahitaji mshambuliaji hilo ndio jambo pekee lililosalia kwenye kikosi cha Yanga sasa, tunahitaji mshambuliaji anayejua kufunga awe anatumia muda mwingi kwenye eneo la hatari.


Yanga imepangwa kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika sambamba na Al Ahly ya Misri, CR Boulizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana na itaanzia mechi zake ugenini dhidi ya Waalgeria na kumalizia pia ugenini ikiwa na kibarua mbele ya watetezi Al Ahly inayoshikilia taji la michuano hiyo kwa mara 11 sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad