Yanga Vs Geita Gold FC Mechi Nyingine Ngumu na Nzuri Kuitazama



GEITA GOLD FC V/s YANGA mechi nyingine ngumu na nzuri kuitazama siku ya leo, Yanga inataka kurudi kwenye njia yake ya ushindi baada ya kupoteza dhidi ya Ihefu. Geita Gold wanaona kama Ihefu waliweza kupata ushindi mbele ya Wananchi kwa nini wao washindwe?

Bila shaka leo Gamondi hatofanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha kwanza badala yake wachezaji walioanzia benchi mechi dhidi ya Ihefu [Aucho, Mudathir, Aziz Ki, Job, Max na wengine ambao walikuwa jukwaani] leo watarejea kikosini.

Geita Gold FC imetoka kuchezea kichapo nyumbani kutoka kwa KMC FC kwa hiyo leo hata matokeo ya sare kwao watayahitaji kuliko kudondosha alama zote tatu.

Kwa hiyo mchezo huu kila timu inautolea macho kwa sababu imetoka kupoteza mchezo uliopita na leo ndio sehemu ya kunyanyukia na kupata faraja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad