Yanga Waomba Tukio la Shabiki wao Kupigwa na Mashabiki wa Simba kuchukuliwa Hatua Kali


Klabu ya @yangasc kesho Oktoba 30, imepanga kuwasilisha barua ya malalamiko na kuomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya mashabiki waliovalia jezi za @simbasctanzania walioonekana kwenye video wakimshambulia shabiki aliyevalia jezi ya Yanga katika Uwanja wa Mkapa.

@simon.esq ameandika; "Mpira ni upendo, kwa kitendo hiki cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga kiasi hiki sio utu kabisaa, hakuna sababu ya msingi ya kumshambulia mtu kiasi hiki. Labda niwakumbushe washamba wote walioshiriki unyama huu, Yanga na Simba ni watani wa jadi sio maadui".

Ameongeza; "Naiomba Bodi ya Ligi Kuu, Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jeshi la Polisi wachunguze suala hili na hatua kali zichukuliwe".

"Klabu itawasilisha malalamiko yake rasmi kesho, na tutaomba hatua kali zichukuliwe kwa huu unyama

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad