Yanga Watamba Kuifunga Azam Leo Kwenye Uwanja Wa Mkapa, Dar

 

Yanga Watamba Kuifunga Azam Leo Kwenye Uwanja Wa Mkapa, Dar


YANGA kwa sasa wapo saiti wakijiandaa kwenda kutafuta ushindi katika mchezo mgumu uliopo mbele yao dhidi ya Azam FC utakaochezwa leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 Yanga Watamba Kuifunga Azam Leo Kwenye Uwanja Wa Mkapa, Dar

Kuelekea mchezo huo, uongozi wa Yanga umesema wapinzani wao Azam watakufa kifo kibaya sana kama ilivyo kawaida yao wanapokutana hasa kwa mechi za hivi karibuni.


Jambo kubwa ambalo Yanga wanalikumbuka kuelekea katika mchezo huo, ni matokeo mazuri waliyoyapata katika michezo mitatu iliyopita dhidi ya Azam FC katika mashindano mbalimbali.


Katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, wafungaji wakiwa ni Fiston Mayele, Aziz ki na Farrid Mussa, huku mabao ya Azam FC yote mawili yakifungwa na Abdul Sopu.


Kwa upande wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports msimu uliopita, Yanga iliifunga Azam bao 1-0, kisha nusu fainali ya Ngao ya Jamii msimu huu, Yanga ikashinda 2-0.


Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Hivi karibuni tumekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Azam FC, lakini hio haifanyi sisi tujiamini sana, kikubwa ni kwamba tunakweda kutafuta matokeo mazuri dhidi yao na tunaamini Azam watakufa kifo kibaya sana,” alisema Kamwe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad