Ahmed Ally 'Kuhusu Mabango Tumesababisha Sisi Kufungwa, Next Time Tufanye Juhudi'


Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Ahmed Ally @ahmedally_ amesema Klabu ya Simba imeyaona mabango yanayoonesha matokeo ya Kariakoo Derby ambapo amesema kitengo cha sheria cha Simba SC kinaangalia kuona kama inafaa kuchukua hatua au kuacha huku akikiri kuwa kadhia hiyo imesababishwa na wao kwa Wachezaji kuruhusu kufungwa bao tano.

Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo, Ahmed amesema “Kuhusu mabango tumeyaona na tuna kitengo cha sheria, wanaangalia kuona kama inafaa kuchukua hatua au kuacha lakini hili tumesababisha sisi, wakati ujao Wachezaji wafanye kila linalowezekana hiyo kadhia isitokee tena, mwiba unatokea ulipoingilia”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad