ALLY Kamwe: Al Ahly Wamekuja Wakati Mbaya, Tunawapiga

 

ALLY Kamwe: Al Ahly Wamekuja Wakati Mbaya, Tunawapiga

Yanga SC wamesema wapinzani wao katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly wamekuja wakati mbaya hivyo lazima waziache alama tatu kwa Mkapa jijini Dar.

Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema Al Ahly amekuja wakati ambao wao wametoka kupoteza goli 3-0 dhidi ya CR Belouizdad na wana mpango wa kuvuna alama zote tatu za nyumbani.

"Wwamekuja wakati mbaya na sisi tunazitaka alama tatu za nyumbani, wamekuja tukiwa tunahitaji ushindi wa nyumbani kurudisha heshima yetu baada ya kupoteza," alisema Kamwe.

Yanga watakuwa na kibarua cha kuwavaa Al Ahly ambao wanaongoza kundi lao wakiwa na alama 3 huku Yanga wakiwa na sifuri sambamba na Medeama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad