Askari Waliomuua Mlinzi wa Bar Watiwa Mbaroni

 
Askari Waliomuua Mlinzi wa Bar Watiwa Mbaroni

Askari waliomuua mlinzi wa Bar watiwa mbaroni

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limepokea taarifa kuwa November 29,2023, usiku maeneo ya Sinza Mapambano Kinondoni Askari wawili walimjeruhi kwa risasi Mtu mmoja aliyefahamika kwa Jina la Razaki Azan mwenye umri miaka 29 Mlinzi binafsi wa Bar iitwayo Board room iliyopo Sinza Dar es salaam ambaye baaade alipoteza maisha.

Jeshi la Polisi limesema tayari limewakamata Askari hao na mambo ya kisheria yanakamilishwa na watachukuliwa hatua za kisheria haraka kadri iwezekanavyo kwa kufuata mifumo ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani.

“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala kukamilisha uchunguzi”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad