Aziz K Awagawa Yanga, Huku Simba Wakimmezea Mate ya Alafi


SIKU chache tangu ifichuke kuwa Simba inammezea mate Stephane Aziz Ki ikitaka aende kukiimarisha kikosi cha Msimbazi, wanachama na mashabiki wa Yanga wa Nyanda za Juu Kusini wametofautiana mtazamo baadhi wakikubali na wengine wakiweka ngumu.

Simba ilifumuliwa mabao 5-1 na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu na kufikia hatua ya kumpiga chini kocha Roberto Oliveira Robertinhoâ aliyeandika ripoti aliyowakabidhi viongozi kwamba wahakikishe wanamsajili Aziz KI kuimarisha kikosi kupitia dirisha dogo litakalofunguliwa mwezi ujao.

Aziz Ki mwenye mabao saba kwa sasa, amekuwa mwiba mkali katika Ligi Kuu na alihusika katika mabao mawili kati ya yale matano yaliyoizamisha Simba Kwa Mkapa kwa 5-1, akifunga moja na kuasisti jingine, lakini wana Yanga baada ya kusikia taarifa hiyo wamegawanyika, huku wakiwataja Fiston Mayele na Bernard Morrison.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga tawi la Tunduma, Songwe, Esau Lwinga ‘Esau Yanga’ alisema timu hiyo inaweza kuendelea kutesa bila ya Aziz Ki au staa yeyote akisema Simba kama wako siriazi waende mezani.

“Mpira ni biashara na hatuwezi kutetereka kwa kumkosa mchezaji mmoja, aliondoka Fiston Mayele, Bernard Morrison, Yannick Bangala na Feisal Salum, lakini tumeendelea kuwa bora, hivyo kama Ki naye wanamtaka waje mezani, labda wakimng’oa Hersi Said,’ alisema Esau Yanga, huku mkereketwa wa Yanga tawi la Mwanjelwa jijini Mbeya, Hashim Jumbe alisema kwa sasa si muda sahihi wa kuuza silaha kwa mpinzani akisema uongozi wa timu hiyo uwe makini.

“Siafiki mchezaji yeyote kuondoka Yanga kipindi hiki ambacho tunakabiliwa na mashindano makubwa haswa wale tunaowategemea akiwamo Aziz Ki, uongozi uwe makini,”€ alisema Jumbe.

Msimu uliopita Aziz KI alimaliza na mabao tisa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad