Baba Levo: Harmonize Sio Mtu Mbaya ila Hana Shukrani

 

Baba Levo: Harmonize Sio Mtu Mbaya ila Hana Shukrani

Msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo amesema kuwa msanii mwenzake ambaye amekuwa kama hasimu wa WCB, Harmonize sio mtu mbaya kama baadhi ya watu wanavyodhani lakini ni msanii ambaye hana shukrani.


Baba Levo amesema kuwa Harmonize ameshindwa kuwashukuru watu kama Diamond Platnumz ambao waliomshika mkono na kumfanya afike alipo leo badala yake amekuwa akiwasema vibaya.


"Mimi sioni kama Harmonize ni mtu mbaya ila ni mshikaji ambaye hanaga shukrani, na hicho ni kitu cha kawaida watu kukosa shukrani kwa watu waliowasaidia.


"Ndio maana tunaambiwa tenda wema uende zako, lakini kwa mimi sioni ubaya wowote wa Harmonize, hatujawahi kusikia kampiga mtu na mimi nakutana na Harmonize mara nyingi mbona hajawahi kunipiga?


"Tukikutana na Harmonize tunasalimiana vizuri tu na sometime anakuwa na mahela anatuonyesha kwamba ana pesa na hizo pesa akiziweka vibaya nazikwapuaga mara mojamoja," amesema Baba Levo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad