Baba Levo: Nimefurahi Mbosso kulimwa adhabu na BASATA

Nimefurahi Mbosso kulimwa adhabu na BASATA

 Baba Levo: Nimefurahi Mbosso kulimwa adhabu na BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Baba Levo amesema yeye ni miongoni kati ya watu waliofurahia Mbosso kufungiwa na BASATA.


“Nimependa alichokifanya Mwana FA kwa akina Mbosso, Whozzu na Billnass. Walipoadhibiwa wakaenda kwake kukata rufaa, akaona hawa vijana wanatakiwa kupata riziki, wanapaswa kulipa tu faini na maisha yao ya muziki yakaendelea, haya ndiyo mambo tunayotaka Mwana FA afanye na sio kusapoti ujinga.


“Kama kuna sehemu mtu amefanya ujinga aadhibiwe, kwa mfano Mbosso aliniudhi sana ile video. Mimi mwenyewe nilikuwa upande wa BASATA, kwenye ile video muonekano wake ulikuwa mbaya japo kuwa ilikuwa acting, ilitakiwa ionekane usiku tu.


“Kwa hiyo hii nyundo aliyopigwa Mbosso ni sawa, alipe pesa za watu ilia ache ule uhanangwa aliofanya mle ndani. Hatupingi kila kitu,” amesema Baba Levo.


Wasanii Oscar Lelo ‘Whozu’, William Lyimo ‘Billnass’ na Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ wamepata ahueni ya kuondolewa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na muziki iliyokuwa imetolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Novemba 4, mwaka huu. Hata hivyo wasanii hao hawatajishughulisha na muziki hadi watakapotekeleza adhabu ya kulipa faini walizotozwa na Basata zilizokuwa zikienda pamoja na adhabu za kufungiwa.


Uamuzi huo umefikiwa Novemba 14, 2023 kwenye kikao kilichoongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro kilichofanyika ofisi za wizara zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu wa wizara Gerson Msigwa na wasanii hao.


Whozu alitozwa faini ya Sh milioni tatu na Basata, lakini kutokana na uamuzihuo atalipa Sh milioni tano, Billnass alitozwa Sh milioni tatu, lakini sasa atalipa Sh milioni moja na Mbosso yeye atalipa Sh milioni tatu. Kulingana na uamuzi wa leo wakitekeleza adhabu hiyo wataendelea na shughuli zao za muziki.


Whozu pia amepewa muda wa saa sita kutekeleza agizo la kushusha wimbo huo kwenye mitandao yake ya kijamii.


Basata ilitangaza kumfungia Whozu miezi sita kutokana na kuchapisha video ya wimbo Ameyatimba aliowashirikisha wasanii hao ambayo inakiuka maadili na ina vitendo vyenye ishara ya matusi. Billnass na Mbosso kila mmoja alifungiwa miezi mitatu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad