Baraza la Maaskofu Katoliki hawana unafiki kwa watawala

 

Baraza la Maaskofu Katoliki hawana unafiki kwa watawala

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima amezungumza katika Mkutano ulioandaliwa na Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu kwa kushirikiana na kamati za dini mbalimbali (CCT, TEC na BAKWATA) kuhusu umuhimu wa uchaguzi kupata viongozi wa kuongoza na mafunzo waliyopata katika nchi walizotembelea mpaka sasa (Tanzania, Kenya na Afrika Kusini).


Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Kenya, Viongozi wa Dini, vyama vya siasa nchini, na wataalamu kutota taasisi mbalimbali nchini.


"Tuliona Afrika Kusini na Kenya, ambapo Kenya Rais alikataliwa alipochoguliwa ambapo uchaguzi ilibidi urudiwe, Afrika Kusini, Thabo Mbeki, Zuma waliondoka madarakani kutokana na ukweli kwamba Tume ni chombo kinasema, "Tunawapa mtu kadiri ya Sheria, na kwa mujibu wa Sheria usiporidhika Sheria hiyo hapo. Tanzania hicho hakipo!


"Ila kuna upande wa Mbunge na Diwani, mmeridhika na matokeo hamjaridhika juu ya utendaji haipo. Wenzetu hata kwenye utendaji, unatenda vizuri au hautendi vizuri, Tanzania mpaka miaka mitano ipite, labda utende kosa la jinai, lakini kama ni makosa ya kawaida, wanachi hawaridhiki- sawa kuna 'probition' (adhabu ndogo/kipindi cha uangalizi), sijui 'impeachment' (kumvua madaraka kiongozi) lakini hatujawah kuona zikifanya kazi!


"Kingine tulichojifunza juu ya majukumu ya Tume, Tume ina majukumu makubwa ya kuandaa watu kushiriki wakiwa na Imani na Tume kwamba tuko kwa niaba yenu kwa mujibu wa Sheria. Kwahiyo ile ‘credibility’ ya Tume imejengwa katika ngazi ya juu sana, na watu wana Imani na Tume Kenya na Afrika Kusini kuliko Serikali yenyewe, na hiyo Imani ni Tuzo nzuri sana, na hakuna kitu ambacho tume hizi mbili zinashughulika kama kuaminika na wananchi, kukubalika, na sio kukubalika tu, KUAMINIKA.


"Maana unaweza kukubalika sababu ukiwabishia unawekwa ndani, au ukifanya jambo fulani unafutiwa usajili, lakini kwa wenzetu wanataka wapiga kura, wapigiwa kura, wanaotunza ustawi wa siasa wan chi wamewekwa vizuri kuwa na Imani na Tume yao, Credible Commissions!


"Sasa ya Tanzania mna Imani nayo ama hamna Imani nayo viongozi wetu na ninyi wenyewe mtatuambia, hilo ndio tuliona la kwanza. Kwahiyo kitu cha kwanza ni kujenga ile haiba ya Tume, usanii sanii kama tunaofanya Tanzania haupo.


"Sijui Uchawa, kujipendekeza pendekeza, kuwa na vikundi vikundi vya kupitisha watu mnapeana madaraka kiujanja ujanja haipo kwenye hizi nchi, labda sehemu fulani huko juu lakini huku chini kwa Diwani na Mbunge imeshafika mahali imeisha!"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad