Bodi ya Ligi Yailaumu Yanga Kutofanya Promo ya Dabi ya Simba na Yanga

Bodi ya Ligi Yailaumu Yanga Kutofanya Promo ya Dabi ya Simba na Yanga


Bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB) imesema haipendezwi na tabia ya timu mgeni kwenye Mchezo wa Kariakoo Derby kutoifanyia promo mechi hiyo na kuachia jukumu hilo kwa timu mwenyeji pekee.


Akizungumza na kituo cha Radio cha Clouds, Msemaji wa Bodi ya Ligi, Karim Boimanda amesema mchezo huo si tu kwa ajili ya mapato ni Mchezo mkubwa Nchini na Afrika mashabiki hivyo vilabu vyote viwili (2) vinapaswa kuipromoti mechi hiyo.


"Hii inatokana na kanuni ya kuwa timu mwenyeji ndio atapata mapato yote ndio maana timu mgeni hafanyi promo, bodi ya ligi hatufurahishwi na jambo hilo tutalifanyia kazi suala hilo. Mechi hii sio tu kwa ajili ya mapato ni mechi ya hadhi ya nchi," amesema Boimanda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad