Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewatoza Wasanii Mbosso @mbosso_ na Billnass @billnass faini ya milioni tatu kila mmoja na kuwafungia kutokujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia leo November 04, 2023 kutokana na Wasanii hao kushirikishwa kwenye wimbo wa ‘Ameyatimba’ ya Whozu @whozu_ , ambao maudhui yake yanatajwa kukiuka kanuni za maadili.
Kwa upande wake Whozu ametakiwa kushusha mara moja video ya wimbo wake wa ‘Ameyatimba’ kwenye digital platform zote, BASATA imemtoza faini ya Tsh. milioni 3 na kumfungia kujishughulisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi 6 kuanzia leo November 04, 2023.
BASATA imesema Whozu alichapisha video ya wimbo huo Nov 02, 2023 akiwashirikisha wasanii wenzake Mbosso na Bill Nass, na kwamba wimbo huo una maudhui yanayokiuka kanuni za maadili kutokana na kuwepo ishara ya vitendo vinavyoashiria matusi kinyume na Kanuni ya 25(6) (j) pamoja na vitendo ya unyanyasaji, ukatili na udhalilisha wa utu wa Mwanamke kinyume na Kanuni ya 25(6)-(f) “Msanii huyu ameshaonywa mara mbili na kutozwa faini mara moja huko nyuma kwa kukiuka taratibu za kuzingatia maadili katika kazi za sanaa lakini bado ameendelea kupuuza”
“Baraza limeshatoa na kuzindua mwongozo wa maadili katika kazi za sanaa ambao unapatikana katika tovuti yetu www.basata.go.tz, hivyo ni jukumu la kila Msanii na mdau wa sanaa kuzingatia maadili katika kazi za sanaa”