BREAKING: Serikali Yatangaza Mtanzania wa Kwanza Kufariki Israel Baada Kutekwa na Hamas


Serikali ya Tanzania imetangaza kifo cha Clemence Felix Mtenga, mmoja kati ya wanafunzi wawili kutoka Tanzania aliyedaiwa kutekwa na Kundi la Hamas kwenye mgogoro unaoendelea huko Gaza.

Katika taarifa iliyotolewa jioni hii na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, familia ya kijana huyo tayari imepewa taarifa hizo.

Marehemu Clemence alikuwa ni miongoni mwa vijana wa kitanzania wapatao 260 waliokwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo chini ya Mpango wa Ushirikiano kati ya Serikali na Israel.

Kwa sasa, wizara tayari imeanza taratibu za kuurejesha mwili wa marehemu Clemence nchini huku mwanafunzi mwingine, Joshua Mollel ambaye naye alipotea Serikali ya Israel inaendelea na jitihada za kumtafuta kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad