BREAKING: Whozu, Mbosso, Billnass wafunguliwa na BASATA

  
BREAKING: Whozu, Mbosso, Billnass wafunguliwa na BASATA

BREAKING: Whozu, Mbosso, Billnass wafunguliwa na BASATA

Kikao cha kusikiliza rufaa ya Wasanii Mastaa nchini Whozu, Billnass na Mbosso kimefikia maamuzi ya kuwataka Wasanii hao kulipa faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi za sanaa nchini kwa kufuata maadili ya Kitanzania.


Maamuzi hayo yamefikiwa kwenye kikao chini ya uongozi wa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro na Naibu Waziri wake Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA kilichofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam.


Whozu anatakiwa kulipa faini ya Tsh. milioni 5, Billnass Tsh. milioni moja huku Mboso akitakiwa kulipa milioni tatu na wote kwa pamoja wameondolewa adhabu za kufungiwa ila wanatakiwa kulipa kwanza kisha waendelee na kazi zao.


Kwa upande mwingine Msanii Whozu amepewa saa sita kutekeleza azimio la kushusha wimbo huo kwenye "digital platforms" zote kama makubaliano yanavyoelekeza.


Waziri Ndumbaro amewasihi Wasanii hao na wengine nchini kutumia ubunifu kwa kufuata taratibu ulioainishwa katika mwongozo wa uzingatiaji maadili katika kazi za sanaa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad