Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeipiga marufuku Klabu ya Simba na kuielekeza kuondoa neno MO FOUNDATION kwenye jezi zake pia kuondoa logo moja ya MO EXTRA na kubaki na moja.
Maelekezo hayo ya CAF yalitilewa siku kadhaa kabla ya mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Asec Mimosa uliopigwa jana na Simba kuambulia sare ya bao 1-1 katika Dimba la Mkapa.
Awali Simba wakati ikitangaza jezi zao kwa ajili ya michuano ya kimataifa, kuliibuka maswali kuhusu uwepo wa logo mbili za Mo Xtra kifuani kulia na tumboni.
Itakumbukwa pia kuwa, Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kupitia kikao chake cha 51 kilichofanyika tarehe 25 Oktoba 2023 iliridhia kulifuta shirika la Mo Foundation kutokana na kutofanya kazi kwa miaka kadhaa kinyume na sheria za Tanzania za usajili wa mashirika yasiyo ya serikali.