Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kushughulikia kikamilifu kero za migogoro kwa kipindi kisichopungua miezi sita.
Kauli hiyo ya chama imetolewa leo Novemba Mosi, 2023 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Paul Makonda alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara jijini Dodoma.
"Chama kinamuelekeza waziri mkuu ndugu Kassim Majaliwa kusimamia kikamilifu suala la kutatua migogoro ya ardhi kwa kuunganisha wizara tatu chini ya wizara mama ya ardhi.
"Wizara ya TAMISEMI inayo migogoro inayotokana na mipaka, Wizara ya Mariasili inayo migogoro inayotokana na mipaka ya hifadhi na wizara yenyewe ya ardhi inayo migogoro ya ardhi.
"Chama kinamtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndani ya miezi sita awe amesimamia na kuratibu kikamili, kuondoa na kufuta migogoro yote ya ardhi inayopelekea wavuvi, wakulima, wafugaji na wananchi kuteseka ndani ya ardhi yao," alisema Makonda.