Che Malone akiri hana mawasiliano mazuri na Inonga

 

Che Malone akiri hana mawasiliano mazuri na Inonga

Beki kisiki wa Klabu ya Simba, Che Fondoh Malone Junior raia wa Cameroon amekiri kuwa wana mapungufu katika safu yao ya ulinzi ndiyo maana wamekuwa wakiruhusu mabao takribani katika kila mchezo.


Che Malone amesema hayo leo Ijumaa, Novemba 24, 2023 kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Baranbi Afrika hatua ya makundi dhidi ya ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast.


"Tumekuwa tunaruhusu mabao kwa kuwa tuna mapungufu kwenye mawasiliano. Kwenye timu ya soka unahitaji kiongozi kwenye kila idara. Tumezungumza na kocha na leo ni mazoezi ya mwisho, bila shaka tutatatua hilo kuelekea mchezo wa kesho (dhidi ya ASEC Mimosas)," amesema Che Malone.


Tangu msimu huu uanze, Simba imecheza michezo 14 ya kimashindano kuanzia Ngao ya Jamii, Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika na African Football League na kuruhusu jumla ya mabao 17.


Simba imeruhusu mabao 11 kwenye Ligi Kuu ya NBC, mabao 3 kwenye CAFCL na mabao 3 kwenye michauno ya AFL huku ikifanikiwa kugunga mabao 24.


Katika Ligi Kuu ya NBC, Simba imecheza michezo 8 ambapo mechi 2 tu ambazo haijaruhusu mabao ni ile ya Dodoma Jiji na Coastal Union wakati mechi nyingine 6 ikiwa imeruhusu kufungwa jumla ya mabao 11.


Katika safu ya ulinzi ya Simba, asilimia kubwa anacheza Che Malone na henock Inonga, hivyo iwapo mabeki hawa wanakosa mawasiliano wao kwa wao ama wao na kipa anayekuwa langoni siku husika, basi ni rahisi kwa mpinzani wao kuwaadhibu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad