Dabi ya Kariakoo ilipigwa kwa Dakika 50 tu

 

Dabi ya Kariakoo ilipigwa kwa Dakika 50 tu

Bado Yanga inashangilia ushindi wake wa mabao 5-1, dhidi ya watani zao Simba wanaoumia kupewa kichapo hicho kikubwa ikiwa ni kama kisasi kwani mei 6, 2012 mnyama alimuadhibisha Mwanajangwani kwa kumchapa 5-0.


Sahau kuhusu dabi hiyo, hivi unajua mechi nzima juzi ilichezwa kwa dakika 50 tu? Usishtuke! Huo ndio muda ambao boli lilitembea.


Kama ilivyo kawaida yetu, Mwanaspoti tuliweka mtu uwanja wa Mkapa aliyesimamia kifaa maalumu ambacho kilikmuwa kina 'stop watch' na kufanya kazi ya kusimamisha muda kila mara mpira unapokuwa haupo mchezoni na kuendelea unapokuwa mchezoni na mwisho wa siku kubaini dakika ambazo mpira ulikuwa mchezoni ni 50 na sekunde 10 tu.


Dakika nyingi zilipotea pale ambapo mpira ulitoka nje, wakati wa kupiga mapigo ya mpira wa kutengwa (Faulo, frikiki, kona,) mpira wa kurusha, mchezaji akiumia, timu ikifanya mabadiliko, na mambo mengine ya namna hiyo ambayo yanalazimisha mechi kusimama.


Katika dakika 50 hizo hizo ambazo mbungi ilipigwa, kipindi cha kwanza mechi ilichezwa kwa dakika nyingi zaidi kwani mpira ulikuwa mchezoni katika dakika 26 na sekunde 49 huku kipindi cha pili ikipigwa kwa dakika 23 na sekunde 21.


Hivyo manne ya Yanga yaliyofungwa kwenye kipindi cha pili yalifungwa kwa muda mchache zaidi kuliko mawili yaliyofungwa kipindi cha kwanza moja likiwa la Yanga na lingine la Simba.


Kwa maana hiyo jumla ya dakika 40 za mechi hiyo mpira ulikuwa hauko mchezoni  na hii ni kawaida duniani kote ila mwisho wa siku zinabaki kuhesabika kama dakika 90 tu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad