Dabi ya Kariakoo Simba na Yanga ipewe Heshima yake Afrika

Dabi ya Kariakoo Simba na Yanga ipewe Heshima yake Afrika.

Dabi ya Kariakoo Simba na Yanga ipewe Heshima yake Afrika

Watani wa jadi Simba na Yanga wanakutana Jumapili katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Zinapokutana timu hizi, mara nyingi shughuli husimama kwa muda kupisha mchezo huo ambao hufuatiliwa na kundi kubwa la watu ndani na nje ya nchi.

Historia ya klabu hizo, mafanikio ambayo kila moja imewahi kupata katika mashindano ya ndani na yale ya kimataifa, ni mambo yanayopelekea mchezo huo kuwa na mvuto na msisimko mkubwa na wa hali ha juu.

Na safari hii mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu kubwa kwa sababu Simba na Yanga kila moja inaonekana kuwa bora na inafanya vyema katika ligi ya ndani huku kila timu ikiwa imetoka kuingia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikumbukwe hii ni mara ya kwanza katika historia kwa timu mbili za Tanzania kuingia kwa pamoja katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na huko nyuma hakukuwahi kutokea kitu kama hicho. Hivyo basi kutokana na uzito na ukubwa wa mechi hiyo, ni vyema kila anayehusika nayo akahakikisha anatimiza vyema wajibu wake ili iweze kuwa na hadhi inayotegemewa na wengi lakini pia kukidhi kiu ya mashabiki wa soka ndani na nje ya Tanzania.

Timu zinapaswa kuonyesha kiwango bora na soka la ushindani linaloendana na nidhamu ya ndani na nje ya uwanja ili kuepuka kulitia doa pambano hilo ambalo limo katika orodha ya mechi bora tano za dabi Afrika. Waamuzi wanapaswa kuzitafsiri na kuzisimamia vyema sheria 17 za mchezo wa mpira wa miguu ili kupatikane matokeo halali na stahiki kutegemeana na kiwango timu zitaonyesha kiwanjani. Mamlaka nyingine nazo zinatakiwa kila moja kuhakikisha zinawajibika vilivyo katika majukumu yao.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad