Dabi ya Kariakoo Unaambiwa Hakuna Sare Jumapili, Lazima Mtu Apigwe Bao

 

Dabi ya Kariakoo Unaambiwa Hakuna Sare Jumapili, Lazima Mtu Apigwe Bao

Hakuna sare Jumapili, Kariakoo Derby lazima mtu apasuke. Hii ni kutokana na kila upande kuwa na uimara katika eneo fulani uwanjani.


Simba ina uimara eneo la ushambuliaji ila ina weakness kuanzia eneo la ukabaji hadi kwenye eneo la uzuiaji.


Yanga inauimara mkubwa kwenye eneo la kiungo ambapo pia ndipo pamezaliza magoli mengi zaidi (16) kati ya magoli (20) waliyofunga ligi kuu Tanzania bara so far.


⚽ Mabao 6 Assists 2— Aziz Ki

⚽ Mabao 5 Assists 2— Max Nzengeli.

⚽ Mabao 3 Assists 3 — Pacome

⚽ Mabao 2 Assists 2 — Mudathir


Pia uimara wa Yanga uko kwenye eneo la Ulinzi ndio timu yenye cleansheet nyingi. Lakini kuna udhaifu kwa washambuliaji wao, Mpaka sasa washambuliaji hao wamefunga magoli (2) tu ligi kuu Tanzania bara.


Ukitazama hizo scenario utabaini kwamba kila timu inaudhaifu na Uimara ambao haufanani. Kwa hiyo kufungana ni jambo ninalotarajia kwa kiasi kikubwa.


Yanga anataka kushinda ili kulipa kisasi, kuepusha gape la point kuwa kubwa mbeleni na kukaa kileleni bila presha.


Simba anataka kushinda ili akae kileleni asiwe na presha atakapoelekea Mkoani Kigoma kuwavaa Mashujaa FC.


Utabiri wako ni upi?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad