Sakata la nyota huyo kuondoka Yanga baada ya msimu uliopita kumalizika liwaacha baadhi ya mashabiki hawaamini kulikoni?
.
“Tuliporudi Tanzania kuendelea na mkataba wa mwaka ule ambao tuliongeza kuna mambo yaliibuka. Kulikuwepo tofauti kati ya meneja wetu mimi na Bangala (Yannick) alipotofautiana na uongozi wa Yanga. Yale mambo yalikuwa mazito ikashindikana kupatikana muafaka kwa haraka.“
.
“Mambo yaliyokuwa yanasemwa sitaki kuyaweka wazi ila yalinivunja nguvu na nikaona bora tufikie hatua ya kuachana. Tukakubaliana na uongozi kusitisha mikataba na tukaondoka,” anasema Djuma
.
“Baada ya kuachana ugumu ukawa kunipa barua ya kuniacha. Nilikuwa tayari na ofa mbalimbali lakini Yanga hawakutaka kunipa barua yangu. Niliambiwa na watu wangu kwamba walidhani ningekwenda Simba. Hatua ile ilinikosesha kupata timu haraka, nilipopewa barua muda wa usajili ulikuwa umekwisha ndio maana sina timu hadi sasa.”😬