Fahyma Atamba: Rayvanny Hanisumbui Hata Akitembea na Wanawake Wengine

 

Fahyma Atamba: Rayvanny Hanisumbui Hata Akitembea na Wanawake Wengine

Mwanamitindo na mfanyabishara, Fahyma amesema kuwa umaarufu wa mpezi wake, rayvanny haumuumizi kichwa kwani hata akitafuta na wanawake wengine bado yeye ndiye mwanamke anayempenda.

Fahyma amesema hayo wakati akizungumza na chombo kimoja cha habari kuhusu maisha yake na mzazi mwenzake huyo ambaye wamerudiana baada ya kutengana kwa muda.

"Mimi tangu nikutane na Rayvanny sijawahi kuwa na ugomvi nae, sikumbuki ni kipindi gani tuliachana tukawa na ugomvi labda nilikufa nimerudi sasa sikumbuki.

"Pia, umaarufu wa Rayvanny haunisumbui kwa sababu hata akiwa na wanawake wengine najua mimi ndio ananipenda zaidi," amesema Fahyma.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad