Haji Manara Ailipua Kampuni ya Simu Kwa Waziri Nape Nnauye 'Watanzania Tunaibiwa Sana'


Haji Manara Ailipua Kampuni ya Simu Kwa Waziri Nape Nnauye 'Watanzania Tunaibiwa Sana'
Ameandika Haji Manara:

My Brother,My friend wa kitambo, Kada usiyeyumba,Mbunge na Waziri mahiri mwenye kujali,Comrade mwenzangu,Binadamu Jasiri na mwenye maono, Hon Nape Moses Nnauye nna salaam zangu kidogo lakini sorry boss, nazileta public ili na wengine wakupe ujumbe pia.

Watanzania tunaibiwa sana na Makampuni mengi ya Simu,Kuna Wizi mkubwa unafanyika hususan kwenye Mabando ya Internet, unaweza kununua kifurushi cha elfu kumi na usiingie hata Instagram au kudownload kitu, saa mbili au tatu, wanakata na kukutumia msg ya eti kifurushi chako kimeisha!!

Sitaki leo kuyataja jina makampuni hayo kwa sababu za kibiashara, na kulinda image zao, lakini kiukweli kunafanyika wizi wa hali ya juu na kampuni nyingi za Simu, ila kuna Kampuni moja inaongoza kwa dhulma kwa Wateja wao, bila shaka unaweza kuijua ( comments zitakupa mwelekeo)

Nakupa mfano hai, jana Mchana nimenunua kifurushi katika kampuni hiyo cha elfu ishirini cha wiki na sikuingia katika Internet coz huo c mtandao nnaoutumia sana, kufika usiku wamekata, ukiwapigia customer service hawana majibu ya kueleweka.zaidi ya kukutaka uelezee eti kama una tatizo lingine wakati la kuibiwa hawajalitatua

Na Nchi hii dhambi kubwa ni kujaribu kutumia post paid, hiyo ndio balaa huo wizi wake, ni kama umeenda kupeleka pesa za kuliwa na Wajanja wa Kampuni hizo.

Nikuombe wewe na Mamlaka zako, tusaidieni hili jambo, nimeandika haya kwa niaba ya Mamilioni ya Watanzania wanaoendelea kupigwa na hawana pa kulalamika.

Kwao wao kutupa Mawasiliano wanadhani ni kutusaidia bila kujua Watanzania wanalipia pesa zao,walau hii la kutowajali wateja linasameheka katika mazingira yetu ya kitanzania, lakini la wizi linaumiza watu wetu ambao wengi wao vipato vyao ni haba.

Hope utachukua hatua stahiki Kama Minister mwenye dhamana na hizo kampuni.

Ubarikiwe kiongozi wangu 🙏🏻🙏🏻

@napennauye @wizarahmth @tcra_tanzania

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad