Hatimaye Clatous Chama Afunguka Kinachoendelea Simba "Tusitupiane Lawama"





Kiungo Mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amesema “Katika nyakati hizi hakuna haja ya kunyoosheana vidole na kutupiana lawama, haitotusaidia kwa namna yoyote ile. Huu ni wakati sahihi wa kushikamana pamoja na kuunganisha mioyo yetu. Twendeni tena leo tukiwa na nguvu moja na kufanya kazi ili kurejea katika ari yetu.”

Chama amesema hayo baada ya kulaumiwa na baadhi ya mashabiki wa timu yake kuwa yeye ni mmoja wa wachezaji waliocheza chini ya kiwango katika mchezo waliopoteza kwa magoli 5-1 dhidi ya #Yanga, Novemba 5, 2023 katika #LigiKuuBara

#Simba inatarajiwa kukipiga dhidi ya Namungo FC, leo Novemba 9, 2023 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
-

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad