Hii Ndio Sababu Kwanini Kundi la Hamas Hawataki Vita ya Moja Kwa Moja na Israel?




Kutokana na kileambapo tunaweza kuangazia ni kwamba , Waisraeli, ambao walikuwa wameanza uvamizi wa Gaza polepole , hivi sasa wameanza kupiga hatua kubwa

Wanajeshi wao 17 wameuawa katika vita, na hiyo ilitokana na makombora kadhaa ya vifaru ambayo yalishambulia maeneo yao.

Jeshi la Israel (IDF) limetoa video kadhaa asubuhi ya leo za wanajeshi katika maeneo yasiyojulikana.

Wanaonekana kuwa karibu zaidi na mji wa Gaza, lakini ni muhimu pia kukumbuka hili ni eneo dogo kabisa.

Wakati wa amani, unaweza kwenda hadi mwa Gaza na kuingia katikati mwa Jiji la Gaza kwa takriban dakika 15 pekee. Lakini, imewachukua wanajeshi la Israeli siku chache kufika kwenye jiji hilo, jambo ambalo linaonyesha kuwa wanasonga polepole.

Ni muhimu kusema kwamba huwezi kulinganisha na vita vya Urusi dhidi ya Ukraine. Haya si majeshi mawili makubwa yaliyosimama na silaha nzito nzito, yakikabiliana moja kwa moja .

Ni kile ambacho wachambuzi wanaita asymmetric warfare, vita vya wanyonge dhidi ya wenye nguvu.

Kwa hivyo Hamas haitajaribu kuwa na vita vya moja kwa moja dhidi ya Waisraeli. Watakachojaribu kufanya ni kuwasumbua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad