Hivi Hili la Mchezaji Che Malone Limekaaje Kitaalamu

 

Hivi Hili la Mchezaji Che Malone Limekaaje Kitaalamu

Beki wa Simba Che Malome, siku ya Jumapili tarehe 05.11.2023 wakati wanakandwa kichapo cha mbwa mwizi kutoka kwaa watani zao Yanga, alionyeshwa kadi mbili za manjano.

Kitu ambacho kilipaswa kupewa card nyekundu, lakini refa na wasaidizi wake hawakuliona hili sijui hawakuwa na kumbukumbu vizuri, Che Malome hakutoka nje kwa adhabu ile, alicheza tu.

Juzi kati, kati ya Mechi ya Simba na Namungo,Che Malome alicheza tena, Simba walimchezesha mchezaji mwenye card nyekundu kwa sababu zipi?

Bodi ya Ligi mko wapi? TFF mko wapi? Wapeni Namungo ushindi wa point tatu na magoli mawili kama kanuni inavyotamka.

Tunachokijua Kuna mjadala unaendelea mitandaoni na pia memba wa JamiiForums.com amehoji kama ni kweli kuna mchezaji wa Simba, Che Fondoh Malone alipewa kadi mbili za njano na akaendelea kucheza katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, Jijini Dar es Salaam, Novemba 5, 2023.

Uhalisia ulivyo Dakika ya 22, mchezaji wa Simba, Fabrice Ngoma alimchezea faulo Stephane Aziz Ki wa Yanga, Refa akapuliza filimbi wakati huo Che Malone alikuwa anaenda kuupiga mpira, kisha akasogea kwa refa kulalamika akidai haikuwa faulo.

Wakati Mwamuzi anatoa kadi ya njano kwa Ngoma, aliyekuwa karibu ni Che Malone akilalamika, hivyo kadi ilienda kwa Ngoma na si Che Malone kama inavyodhaniwa.

Hata hivyo, Dakika ya 85, Wakati Yanga imepata penati, Che Malone akawa anaonekana analalamika muda mrefu kwa Mwamuzi akilalamikia uamuzi wake, ndipo Mwamuzi akageuka na kumpa kadi ya njano Che Malone.

Hivyo, si kweli kuwa Che Malone alipewa kadi mbili za njano ndani ya mchezo.

Mchezo huo wenye kubeba hisia za wapenzi wengi wa Soka ndani na nje ya Tanzania uliisha kwa Simba kupokea kipigo kikali cha goli 5-1.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad