Hukumu ya Mjane Aliyekutwa na Nyama ya Swala Gumzo

 

Makonda: Mniombee niwe sauti ya wanyonge« NyumaMbele »Comments (0) WhatsApp Facebook Twitter Email This Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amewaomba wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kumuombea awe mwaminifu, mwenye busara na sauti ya wanyonge katika utekelezaji wa majukumu yake.  Makonda aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana Oktoba 22, 2023 jijini Dodoma, akichukua nafasi ya Sophia Mjema aliyeteuliwa kuwa mshauri wa rais katika masuala ya wanawake, watoto na makundi maalumu.  "Mniombee nisiingie katika hili jopo nikabweteka, nikasahau...nyinyi ndugu zangu maisha yangu ndio maisha yenu. Mkienda kanisani na msikitini mwambie Mungu tumemtuma Makonda mkumbuke na umpe hekima, busara na msaidizi mzuri wa Rais Samia (Suluhu Hassan)," amesema Makonda.  Ameeleza hayo leo Jumamosi Novemba 11, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa mji wa Katoro wilayani Geita aliposimama kuwasilimia akielekea Geita mjini.  Tangu kuanza kwa ziara yake, Novemba 9, 2013, Makonda amekuwa akisimama na kusikiliza kero au kupokea taarifa za maeneo husika na kuwapigia simu mawaziri ili kusaka ufumbuzi au majibu ya changamoto zinazowakabili wananchi.  Makonda amesema uzuri wenyewe ana baraka za bosi wake, Daniel Chongolo (katibu mkuu wa CCM), aliyemtaka kuchapa kazi bila hofu wala uoga wowote au kutishwa.  Katika hatua nyingine, Makonda amewaaambia WanaCCM wa mikoa ya kanda ya ziwa kuwa wana deni kubwa la kuhakikisha Rais Samia Suluhu Hassan anapata kura za kutosha zitakazomwezesha kuwa Rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.  Amewataka wananchi wa mikoa ya Kagera, Tabora, Mara, Shinyanga, Geita, Mwanza na Simiyu kumuunga mkono Rais Samia katika jitihada anazozofanya za kuhakikisha Serikali inawapelekea maendeleo kwenye sekta mbalimbali za afya, elimu na miundombinu ya barabara.  Katika maelezo yake, Makonda amesema Serikali inajitahidi kuteleleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kutatua changamoto za Watanzania wakiwemo wa kanda ya ziwa hivyo, aliwataka kutomuangusha Rais Samia katika mchakato wa uchaguzi ujao.  "Nimepewa hii nafasi (uenezi na itikadi), sio kwamba nipo peke yangu,bali nimepata nikiaminiwa kuwa nipo na nyinyi (wananchi).Ombi langu wananchi wa kanda ya ziwa haya mapokezi mlionipa ni ishara tosha Rais Samia hakukosea kunipa nafasi hii hivyo tusimuangushe.  "Kwa tasfiri nyingine tunalo deni la kuhakikisha tunaifanya vema kazi ya CCM, ukiwa na ndugu yako ni rahisi mambo kwenda sasa mimi ndugu yenu nimo.Nina deni kubwa kwa Rais Samia la kuhakikisha ninamlinda na kumtetea na wananchi wa kanda ya ziwa tuna jukumu la kumuombea," amesema Makonda.  Akizungumza kwa niaba ya wabunge na wananchi wa mkoa wa Geita, Mbunge wa Chato, Dk Medard Kalemani amesema pamoja na Serikali kutekeleza masuala mbalimbali lakini Katoro bado kuna shida ya maji, akimuomba Makonda kuwasaidia.  "Tumepata fedha nyingi lakinj yapo mambo mawili ya kukueleza ili ukipata nafasi uyasukume, hapa kuna shida ya kidogo ya maji. Ukipata nafasi tusukumie kwa watendaji waingie site ili maji yaanze kumiminika katika mitaa ya Katoro na Buseresere," amesema Dk Kalemani.  Kama ilivyo kawaida au staili yake ya mzege halilali, Makonda alimpigia Aweso alisema moja changamoto ya Katoro na Buseresere ni upatikanaji wa maji safi na salama, lakini aliwahakikishia Serikali inafanya kazi na kuna mradi wa Sh 6 bilioni ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 92.  "Naomba unipe wiki tatu wana Katoro na Buseresere watakunywa maji safi na salama yenye kutosheleza," amesema Aweso kwa simu huku Makonda akitaka kuwa na uhakika na ahadi hiyo, lakini waziri huyo alisisitiza kuwa watapata maji kwa muda huo.  Naye, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema Rais Samia alipita eneo hilo mwaka jana katika ziara ya mkoa huo na moja kero iliyotolewa na wananchi ni taa za barabarani, lakini hivi sasa zimeshawekwa kwa kilomita mbili.  "Lakini eneo jingine lililoombwa na wananchi ni uboreshaji wa barabara za mtaani, ninachotaka kuwaahidi wananchi ahadi ya Rais Samia itatekelezwa na wataalamu wameshaelekeza kuanza upembuzi yakinifu," amesema Shigela.

Mjadala mkali unaoendelea ni hukumu ya kifungo cha miaka 22 jela alichopewa Maria Ngoda kwa kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala, huku gumzo likiwa ni adhabu aliyopewa kama ilikuwa ni sahihi kisheria ama la.


Ngoda, mkazi wa Isakalilo wilaya ya Iringa, inaelezwa ni mjane, alihukumiwa kifungo hicho Novemba 3, 2023 na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Saidi Mkasiwa baada ya kumtia hatiani kwa kosa hilo.


Ilielezwa na upande wa mashitaka kuwa Novemba 19, 2022, katika eneo la Isakalilo, Ngoda alikutwa na vipande 12 vya nyama ya swala vyenye thamani ya Sh904,757 kinyume cha sheria ya uhifadhi wanyamapori.


Wakili mashuhuri nchini, Method Kimomogoro, alisema tatizo la Tanzania hata kabla ya Uhuru na baada ya Uhuru, ni kwa Bunge kutunga sheria kali za kulinda wanyamapori bila kuzingatia haki za binadamu kwa wananchi wanaoishi jirani.


“Kwanza ngoja nikuambie kitu kimoja ambacho ni kikubwa zaidi kwenye hilo suala. Ni kwamba watu wanaojali uhuru wa binadamu huwa wanaweka categories (makundi) ya makosa ya jinai,” alisema wakili Kimomogoro na kuongeza:


“Kwamba ni makosa gani yapewe adhabu ya kifungo na yapi mtu uanze na faini mara ya kwanza, mara ya pili labda kifungo ni unapokutwa na hatia mara ya tatu. Kwa mfano, makosa ya usalama barabarani mengi unaanza na faini. Mtu akiua swala ambacho ni kitoweo kimeumbwa na Mungu, kwa nini kosa la kwanza afungwe? Makosa ambayo yalitakiwa yawe kifungo bila faini ni yale ya uwindaji wa biashara," alisema na kuongeza kuwa:-


"Bunge letu limekosea, tangu enzi ya mkoloni wao wanaweka adhabu bila kujali hili kosa lina madhara gani,”


Kwa upande wake, wakili Frank Robert alisema kifungu hicho cha 86 (2) (c) (ii) alichoshitakiwa nacho, thamani ya nyara haizidi Sh1 milioni, hivyo ni faini mara tatu ya thamani ya nyara au kifungo kisichozidi miaka 20 jela.


“Sasa hapa ili tujue mama alipata kifungo stahiki au la ni lazima tuone charge sheet (hati ya mashitaka) iliweka vifungu gani maana kama ni 86(1)(2)(c)(ii) basi adhabu inayotajwa ndio hiyo niliyosema.


"Nione kwanza charge sheet,” alisema. Hata hivyo, hukumu hiyo imefafanua kuwa kwa vile sheria hiyo inasomwa pamoja na kifungu namba 60(1) na (2) cha sheria ya Uhujumu uchumi, mahakama imechukua adhabu ya kifungu hicho kati ya miaka 20 na miaka 30.


Wakati mawakili hao wakieleza hayo, tayari makundi na taasisi, ikiwamo Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Kanda ya Iringa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na watetezi wa haki za binadamu wamejitokeza kumsaidia kukata rufaa.


Lakini mbali na makundi hayo kujitokeza, katika mitandao ya kijamii, baadhi ya wachangiaji wamekuwa wakilinganisha hukumu mbalimbali na ya Ngoda na wengine wakifananisha na adhabu kwa vigogo wa ufisadi wa mabilioni. Ushahidi ulivyokuwa


Shahidi wa kwanza, Askari wa wanyamapori anayefanya kazi na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) alisema siku hiyo ya tukio alikwenda eneo la tukio akiwa na watu wengine, akiwemo askari mwenzake, Philomon Wambura.


Kabla ya kufika eneo hilo waliungana na askari polisi John Shayo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Isakalilo, Maisha Modest na walifika eneo hilo saa 8:15 na kumkuta Ngoda akiwa na ndoo nyeupe na ilipofunguliwa ilikutwa na nyama hiyo.


Kwa upande wake, Askari polisi mwenye namba G 4395 Koplo Lubeya aliiambia mahakama kuwa yeye ndiye alipewa jukumu la kumhoji na kuandika maelezo ya mwanamke huyo na baadaye kielelezo kiliteketezwa kwa amri ya mahakama.


Shahidi wa tatu, Mkunde Maleko ambaye ni askari wanyamapori kutoka TAWA, yeye ndiye alipewa vipande 12 vya nyama hiyo ya swala na aliitambua kuwa ni ya swala na alifanyia tathmini ya thamani na kubaini ni Sh904,757.1.


Kwa upande wake, shahidi wa wa upande wa mashitaka, Maisha Modest ambaye ni mwenyekiti wa kijiji alisema siku hiyo alipokea simu kutoka kwa polisi, John Shayi akimtaka wakutane na alipokwenda alimkuta na watu wengine watatu.


Baada ya kumtambulisha kwa watu hao, walikwenda katika nyumba ya mama Ziada Mpiluka na walikuta watu ambapo walijitambulisha na katikati ya watu hao walikutana na Ngoda akiwa na ndoo nyeupe ikiwa mbele yake.


Alitakiwa kufungua ndoo hiyo na alipoifungua, yeye aliona vipande 12 vya nyama na alipoulizwa ni ya mnyama gani hakuwa anafahamu, bali yeye alipewa tu na mwanamke mwingine aliyemtaja kwa jina la Kibuna Fute ili aiuze.


Yeye pamoja na timu hiyo ya maofisa wanyamapori ilikwenda hadi nyumbani kwa Kibuna lakini hawakumpata na ndipo Ngoda alipokamatwa na maofisa hao na Polisi waliokuwa wamefuatana na kujaza fomu ya kukamata nyama.


Shahidi wa tano ni Koplo Owago wa Jeshi la Polisi mwenye namba F 8404 na ndiye alikuwa mtunza vielelezo ambaye alisema Novemba 20, 2022 alipokea kielelezo cha nyama ya swala ambapo aliandaa nyaraka zilizowezesha kuteketezwa.


Kwa upande wake, shahidi wa sita, WP Koplo Agnes alisema kwamba akiwa kituoni alimpokea ofisa mmoja wa TAWA akiwa na Ngoda akiwa na kielelezo cha vipande 12 vya nyama ya swala ambayo Ngoda alielezwa kukamatwa nayo.


Utetezi wa Ngoda ulivyokuwa Katika utetezi wake, mwanamke huyo alieleza kuwa ni kweli alikamatwa katika eneo hilo linalotajwa na upande wa mashitaka akiwa na ndoo ya plastiki na kwamba awali alimkuta mwanamke mwingine akiwa na ndoo hiyo.


Baadaye mwanamke huyo alimuaga kuwa anakwenda nyumbani kuchukua pesa, lakini baada ya dakika 15 tu kupita, aliona watu waliofutana na mwenyekiti wa kijiji wakija eneo lake na walimweleza wanatilia shaka kilichopo ndani ya ndoo.


Walimwambia aifungue ndoo hiyo lakini akakanusha kuhusika nayo na kuwaambia kuwa ndoo hiyo ni mali ya Kibuna Fute na walimtaka awaonyeshe alipo, lakini akawaambia alikuwa amemwaga kuwa anakwenda nyumbani.


Aliwaambia maofisa hao kuwa mwenyekiti anamfahamu mwanamke huyo pamoja na nyumba anayoishi, aliambiwa afungue ndoo hiyo na baada ya kufunguliwa kwa ndoo hiyo, maofisa hao walimweleza kuwa yeye ndiye mmiliki wa nyama hiyo.


Hukumu ya mahakama Katika hukumu yake, pamoja na ushahidi mwingine, mahakama iliegemea maelezo ya ungamo yanayodaiwa yalitolewa na mshitakiwa mwenyewe kwa hiari yake akikiri kukutwa na vipande hivyo 12 vya nyama ya swala.


“Nakumbuka mnamo tarehe 19/11/2022 majira ya saa 8:15 katika mtaa wa Isakalilo Kata ya Isakalilo Manispaa Iringa wakati nipo kwa mama Ziada nilikuwa nauza nyamapori lakini hakunitajia ni nyama gani,” anaeleza.


“Vilikuwa ni vipande 13 na kimoja alichukua lakini nilivyokamatwa navyo ni 12 vya nyama pori ambavyo nilipewa na Kibuna Fute ili nimuuzie,” alinukuliwa Ngoda katika maelezo ya onyo aliyoandika polisi.


Hakimu Mkasiwa alisema katika maelezo yake hayo, mshitakiwa alikiri kukutwa na vipande hivyo 12 vya nyama ya swala na akashindwa kuonyesha shaka yoyote kwa ushahidi wa upande wa mashitaka uliotolewa mahakamani.


“Lakini pia mshitakiwa alishindwa kuwahoji kikamilifu mashahidi wa upande wa mashitaka kuhusiana na ushahidi wa kukutwa na vipande hivyo 12 vya nyama ya swala. Ni sheria, kama shahidi hakuhojiwa ushahidi wake unapokelewa,” alisema.


“Hivyo upande wa mashitaka umeweza kuwasilisha ushahidi wa kutosha kuwa mshitakiwa alipatikana na vipande 12 vya nyama ya swala ambavyo ni nyara za serikali kinyume cha sheria,” alieleza Hakimu Mkasiwa katika hukumu yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad