Kibu Denis Afunguka Kuondoka Robertinho, Atuliza Mashabiki




WAKATI aliyekuwa kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, anatua Msimbazi, alimtaja Kibu Denis kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi ndani ya kikosi hicho na kumpa zawadi, na baada ya hapo kazi iliendelea huku staa huyo akitakata katika utawala wake.

Kibu chini ya Robertinho alikuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza na kuweza kuonyesha ubora wake uliowakosha mashabiki na wadau wa soka waliomchukulia poa mwanzo, lakini baada ya kuondoka kwa kocha huyo baadhi ya mashabiki wamekuwa na wasiwasi juu ya uwezo wa mshambuliaji huyo huku yeye akisema waondoe shaka.

Kibu ambaye amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ inayojiandaa na mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger na Morocco, alisema anaamini katika uwezo wake na siyo kubebwa kama wengi wanavyodhani.

“Siamini kwenye kubebwa, bali kupambana na kuonyesha kitu kila ninapopata nafasi,” alisema Kibu na kuongeza:


“Soka ni mchezo wa wazi na kila mtu anaona, hivyo sitaki kuongea mengi kwani kazi yangu ni kucheza na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi, hivyo naamini nitaendelea kufanya hivyo kila nikipata nafasi.”

Supastaa huyo anamudu kucheza winga zote mbili na eneo la ushambuliaji wa kati, ambapo katika msimu huu ameihusika kwenye mabao matatu ya Simba katika Ligi Kuu akifunga moja na kutoa pasi za mwisho ‘asisti’ mbili.

Kibu alijiunga na Simba akitokea Mbeya City mwanzoni mwa msimu uliopita lakini kabla ya hapo aliwahi kuzichezea klabu za Geita Gold na Kumuyange FC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad