Kipa Aishi Manula Aipasua Simba Dabi ya Kariakoo
Presha imezidi kuongezeka kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi, ni baada baadhi ya viongozi wa Simba SC kumtaka Mlinda Lango chaguo la kwanza Aishi Manula akae langoni kuchukua nafasi ya Ally Salim.
Dabi hiyo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki, wadau wa soka kutokana na ubora wa kila timu, huku mchezo ukitarajiwa kupigwa Jumapili (Novemba 05) kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Manula ameshapona maumivu yake ya nyama za paja, ni baada ya kufanyiwa operesheni nchini Afrika Kusini alipoenda mwishoni mwa msimu uliopita.
Mmoja wa Viongozi wa Benchi la Ufundi la timu hiyo, amesema kuwa wapo baadhi ya viongozi wamependekeza Manula aanze katika mchezo huo huku wengine wakishauri aendelee kukaa Salim.
Kiongozi huyo amesema kuwa, wanaotaka Manula aanze, wenyewe wanaamini uzoefu utamuwesha kukaa golini kutokana ugumu wa mchezo huo, ambao wapinzani wao wapo bora kuanzia safu ya kiungo ya ushambuliaji
Ameongeza kuwa Salim ni mzuri, lakini amekosa uzoefu ambao umewasababishia waruhusu bao golini kwao kwa kila mchezo wanaoucheza.
Mashabiki Chelsea waingia hofu EPL
“Tunakwenda kukutana na Young Africans ambayo hivi sasa ni bora, kila sehemu na mbaya zaidi wana viungo washambuliaji watakaoweza kuamua mechi katika mchezo huu.”
“Kila kiungo mshambuliaji ana uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi ya bao, hivyo ni lazima tuingie kwa tahadhari kubwa, licha ya Manula kutocheza mchezo wowote mgumu zaidi ya ile ya kirafiki tuliyocheza Uwanja wa Simba Mo Arena (Bunju).
Uzoefu wake wa kucheza mechi nyingi za Dabi, ndio utakaomfanya Manula aanze katika kikosi cha kwanza, Salim shida yake anakubali kuruhusu bao katika kila mchezo;” amesema kiongozi huyo.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amezungumzia hilo kwa kusema kuwa: “Kweli kabisa tunakwenda kukutana na Young Africans ambayo ipo katika ubora wake, hivyo ni lazima tuingie kwa tahadhari kubwa kuelekea mchezo huo.