Klabu ya Manchester United imepata pigo baada ya majeruhi wapya ya Rasmus Hojlund na Christian Eriksen baada ya ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Luton Town, juzi Jumamosi (Novemba 11).
Hojlund alitolewa kipindi cha pili na tatizo la misuli ya paja huku Eriksen akilazimika kutolewa nje katika kipindi cha kwanza kutokana na jeraha la goti.
Ni habari mbaya zaidi kwa kocha Erik ten Hag, ambaye tayari hana Casemiro, Lisandro Martinez, Luke Shaw, Tyrell Malacia na Jonny Evans.
Aaron Wan-Bissaka alikosa mchezo dhidi ya Luton kwa sababu ya Ugonjwa huku Jadon Sancho akisalia nje ya kikosi cha kwanza kwa sababu ya suala la kinidhamu.
“Kwa wakati huu Siwezi kusema chochote kuhusu hilo jeraha la Hojlund kwa sababu sijui,” alisema Ten Hag mara baada ya mchezo wa Jumamosi.
“Tunafanya tathmini, lakini inabidi tusubiri kwa saa 24 ili kuona hitimisho ni nini. tuwape madaktari wa timu saa 24 kuona tatizo ni nini, kama kuna tatizo.”
Kuachwa kwa muda mrefu kwa Hojlund, ambaye amejiweka kuwa chaguo la kwanza la mshambuliajà wa United baada ya uhamisho wake wa Pauni Milioni 72 kutoka Atalanta msimu wa majira ya joto, itakuwa pigo kubwa kabla ya mechi ngumu za Ugenini dhidi ya Everton, Galatasaray na Newcastle United baada ya mapumziko ya kimataifa.
“Hatutaki kupoteza mchezaji yeyote na ni sawa kwa Christian Eriksen, lakini huu pia ni msimu wetu, majeruhi wengi,” Ten Hag aliongeza.
“Kwa hiyo una kikosi. Lakini tunazungumza mara nyingi, viwango vya kawaida katika timu yako, katika njia ya uchezaji. Tunatumaini wachezaji wanarejea.
Marcus Rashford, ambaye amefunga bao moja pekee katika michuano yote msimu huu, na Alejandro Garnacho wote walipoteza nafasi nzuri.