Kocha Robertinho Amshauri Mohammed Dewji ‘Mo’ Amng’oe Aziz Ki Pale Yanga.


Kuna siri moja Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amewaachia Simba. Kwenye ripoti yake aliyoacha amemwambia Mohammed Dewji ‘Mo’ amng’oe Aziz Ki pale Yanga.

Amekiri kumwambia mchezaji huyo ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni Yanga ni mashine na kila alipokuwa akikutana nae alikuwa roho mkononi.

“Nilimpendekeza Aziz kwa kuwa tayari yuko Tanzania ameshaanza kuzoea mazingira mazuri ni tofauti na mchezaji mpya anayefika kuja kuanza kuzoea mazingira ya hapo,” amefunguka kocha huyo.

Robertinho amesema kama angeambiwa staa mmoja wa haraka kumchukua ndani ya kikosi cha mabingwa hao basi angekuwa Aziz Ki pekee na kama kuna bahati kubwa kwa watani wao ni kuwa na mchezaji bora kama raia huyo wa Burkina Faso.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad