Kocha Mkuu wa Taifa Stars Adel Amrouche amesema Jana amefanya mabadiliko ya Kikosi kwa kuwaweka nje wachezaji Kama Mbwana Samatta, Simon Msuva, Aishi Manula na wengine ilikuwa ni kuwapa nafasi vijana wengine kuonesha walichokuwa nacho kabla ya kwenda kwenye mashindano ya AFCON nchini Ivory Coast, mwezi Januari.
Amrouche alisema: “Sio kila siku Mbwana Samatta au Simon Msuva, mechi dhidi ya Niger tulitumia nguvu nyingi sana kwa hivyo kwenye mchezo dhidi ya Morocco nifanye mabadiliko katika Kikosi changu ndio maana nimewaweka nje kwanza Samatta na Msuva.
“Lakini pia sio kwa bahati mbaya nimewaweka nje kwa ajili ya kuwaangalia wachezaji wengine na uwezo wao kwa ajili ya AFCON mwezi Januari, kama siku zote wanacheza wao nitawajuaje wachezaji wengine kwenye mechi wanakuaje na hii itanisaidia kujua kikosi changu cha AFCON.
“Maana hatuna muda wa michezo mingi ya Kirafiki kwa hivyo Kuna muda najaribu wachezaji wengine kwenye mechi ya mashindano.”- amesema Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche.
“Lakini pia Aishi Manula bado hajapona vizuri kwa hivyo nimeona ni bora apunzike niweke mlinda mlango mwingine ila naamini mmeona namna timu ilivyocheza na hapa nikipata mechi moja au mbili kwenye Kalenda ya FIFA tutakuwa vizuri kwa ajili ya AFCON.