Kupima DNA Bongo ni Laki Kila Mmoja, Hizi Ndio Taratibu za Kufuata

Kupima DNA Bongo ni Laki Kila Mmoja, Hizi Ndio Taratibu za Kufuata

Kupima DNA Bongo ni Laki Kila Mmoja, Hizi Ndio Taratibu za Kufuata

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema matokeo ya uchunguzi wA DNA (kuhakiki uhalali wa Watoto kwa Wazazi) ni ya uhakika na kwamba gharama ya uchunguzi ni Tsh. Laki moja kwa sampuli ya Mtu mmoja hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla ni Tsh. Laki 3 na malipo yote hufanyika Benki.


Akiongea leo November 30,2023 Jijini Dar es salaam Mkemia Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dr. Fidelis Mafumiko amesema ili kupata huduma ya uchunguzi zipo taratibu za kuzifuata ambapo Mteja haendi moja kwa moja kupima DNA ila anawakilishwa na Taasisi zilizotajwa kisheria ili kumuombea Mteja huduma ya uchunguzi, Taasisi hizo ni Ustawi wa Jamii, Mawakili, Mahakama, Jeshi la Polisi kwa masuala yanayohusu jinai n.k.


“Taasisi hizo zitaandika barua ya maombi ya kupatiwa huduma kwa niaba ya Mteja husika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, na baada ya kulipia gharama sampuli zitachukuliwa na uchunguz
i utafanyika na majibu yatatolewa kwa Taasisi iliyoandika barua ambapo Mteja atapata majibu kupitia Taasisi hizo ndani ya wastani wa siku 27 za kazi (kutegemea na aina ya sampuli).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad