Mafuriko Yauwa zaidi ya 30, Serikali Yatoa Tahadhari



Mafuriko Yauwa zaidi ya 30, Serikali Yatoa Tahadhari

Waziri wa Habari wa Somalia, Daud Aweis amesema Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo zimesababisha mafuriko makubwa yaliyowaua watu zaidi ya 30.

Aweis amesema watu takribani laki 500,000 wameyahama makazi yao kutokana mafuriko na kuonya kwamba wengine zaidi ya milioni moja huenda wakaathirika.


Uharibifu mkubwa umeshuhudiwa katika mkoa wa Gedo, ulioko kusini mwa Somalia pamoja na Mkoa wa kati wa Hiran ambako kingo za Mto Shabelle zimevunjika na barabara kusombwa na maji katika mji wa Beledweyne.

Taifa hilo la pembe ya afrika limekumbwa na mvua kubwa isiyoisha tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba, kutokana na hali ya hewa na ujio wa mvua za El Nino.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad