Makamu wa Rais wa Yanga ashinda tuzo ya CEO Bora UK




Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Ally Haji ambaye pia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Bima la Zanzibar ZIC ameshinda tuzo ya Insurance Corporation CEO of the Year 2023 (Afisa Mtendaji Mkuu bora wa Shirika la Bima 2023).

Tuzo hizo ambazo zinatolewa na jarida la Global Brands la United Kingdom (UK), Arafat ameshinda katika kipengele cha Leadership Awards.

Mbali na Arafat kushinda tuzo hiyo, ameliongoza Shirika la Bima la Zanzibar kushinda tuzo ya Most Reliable Insurance Corporation katika kipengele cha Insurance Awards.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad