Mambo Yalianza Kuwaaribikia Simba Baada ya Kibu Denis Kuumia



Binafsi naona mambo yalianza kuharibika kwa Simba baada ya Kibu kuumia na kulazimika kutoka, mpira ulipoanza tu Yanga walipata goli lililoanzia upande wa kushoto wa Simba baada ya Yanga kufanya shambulizi ambalo liliokolewa lakini kwa haraka Yanga wakatengeneza shambulizi jingine wakafunga.

Baada ya goli lile la Yanga, Kibu Denis alihamia upande wa kushoto wa Simba kusaidiana na Mohamed Hussein, baada ya hapo Yao akawa hapandi tena mara kwa mara kwenda hadi mwisho wa uwanja kwenye eneo la Simba.

Ukiangalia magoli mengine manne ya Yanga ambayo yakianza kupatikana kuanzia dakika ya 64, magoli matatu yametokea upande wa kushoto wa Simba ambako Kibu alikuwa anasaidia sana kukaba kabla hajatoka.

- Yahaya Mohamed 'Mkazuzu'

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad