Mangungu, Try Agin Wapewa Saa 24 Kujiuzulu Simba
Mashabiki wa Klabu ya Soka ya Simba wanaandaa maandamano kupinga baadhi ya viongozi wanaosimamia klabu hiyo wakiwemo Mwenyekiti wa Klabu Murtaza Mangungu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Abdallah Salim 'try Agin' wakiwataka wajiuzulu..
Haya yanajiri baada ya Simba kupoteza michezo wao wa Jumapili dhidi ya watani zao Young Africans ambapo Simba walipigwa bao 5-1, mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa saana kuhusiana na viongozi hao.
Majina ya Mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu pamoja na Salim "Try Again" yamepewa kipaumbele zaidi katika maandamano hayo ambapo wamepewa saa 24 kujiuzulu.
Simba itautumia uwanja wa Uhuru hii leo kwenye mchezo wa Ligi kuu Nchini Tanzania dhidi ya Namungo Fc mwendo wa saa 10 kamili Jioni. Mashabiki hao wamejiandaa tiyari kwa Mabango kuelekea mwenye mchezo huo.
“Tunawapa saa 24 wahakikishe kwamba wametuachia klabu yetu, Simba tuna nyimbo zetu, wasipotusikia tutaziimba nyimbo zetu.
“Sasa hivi tunawaomba wajiuzulu kwa hiari, wakikataa titaimba nyimbo zetu tunazijua, tukiimba wao wenyewe wataenda kwenye vyombo watasema tumeshindwa. Sasa wasingoje tukaimba nyimbo zetu, waachie wenyewe kwa hiari.
“Huyu Try Again uwezo wake wa kushirkkisha watu uko chini kabisa, hataki. Utaendeshaje klabu wewe mwenyewe na Mangungu tu? Tunachokisema, bora wajiuzului kwa maslahi ya Simba, ni bora wajiuzulu kwa kutunza heshima zao.
“Simba sio klabu ya kwenda kufungwa bao tano kirahisi namna ile, mchezaji anapoteza mpira anacheka, hamna hata mtu wa kumuuliza baada ya mechi kwamba mbona ulikuwa unacheza namna ile?,” wamesema mashabiki hao.