Matajiri 8 Waitana Yanga Fasta mchezo wa Kariakoo Dabi Jumapili hii



YANGA wanaonekana kuutaka mchezo wa Kariakoo Dabi, ni baada ya Kamati ya Mashindano ya timu hiyo, yenye watu nane imepanga wamekutana Jumatano kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi kuelekea mchezo huo.

Dabi hiyo inatarajiwa kuzikutanisha timu hizo kongwe za Simba dhidi ya Yanga ambayo itapigwa Jumapili hii saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kamati hiyo ya mashindano, inaongozwa na Matajiri wakubwa hapa nchini wakiongozwa na Mwenyekiti, Rogers Gumbo, Seif Magari, Mustapha Himba, Lucas Masahauri, David Mosha, Majid Suleiman, Pelegrinus Rutayuga pamoja na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said mwenyewe.

Taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, matajiri wamepanga kukutana kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi kabla ya kufanya kikao na wachezaji siku moja kabla ya mchezo huo.


Mtoa taarifa huyo alisema kuwa katika kikao, kikubwa kitakachojadiliwa kuiandaa timu sambamba na kuwapa hamasa na morali itakayowafanya wacheze kwa kujituma ili wapate ushindi.

Aliongeza hamasa hiyo itakwenda sambamba na kuweka bonasi ya wachezaji kabla ya kukutana na wachezaji kuwatangazia ahadi hiyo ya fedha waliyokubaliana wawatangazie ili wapambanae katika mchezo huo.

“Ili tuwape ugumu wa ubingwa wa ligi wapinzani wetu Simba, basi ni lazima tuwafunge Simba tutakapokutana nao ili tujiwekee mazingira mazuri ya kulitetea taji letu la ligi.

“Hivyo viongozi wamepanga kukutana haraka kesho (leo Jumatano), kwa ajili ya kusuka mikakati ya ushindi kuelekea Dabi hiyo, ambayo Kamati ya Mashindano inauhitaji mchezo huu kwa ajili ya ushindi.
“Ni mechi ambayo inakwenda kuamua hatima ya ubingwa wa ligi, hautakuwa mchezo mwepesi kwetu, kwani wapinzani nao wanahitaji ushindi ambao ni ngumu kuupata,” alisema mtoa taarifa huyo.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Muargentina Miguel Gamondi alizungumzia mchezo huo wa dabi kwa kusema kuwa: “Wanakwenda kucheza mchezo mwingine mgumu, ambao ni lazima tupate ushindi licha ya huo ugumu.

“Yanga kwetu kila mchezo ni mgumu, kwani kila timu inayotaka kukutana na sisi inaingia kwa kucheza kwa kupania, hivyo tumejiandaa na mchezo huo wa Dabi kuhakikisha tunaendelea na kasi yetu ya ushindi msimu huu baada ya kuzifunga Azam FC na Singida Fountain Gate.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad